MUNGU BABA ANAKUWAZIA MEMA

 

YER.29.11 Inasema; Maaana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi,asema Bwana , ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Maneno haya yalitamkwa na Bwana Mungu wetu akiwahakikishia Israeli kuwa yale anayowawazia  ni mawazo mema kabisa. Hana mpango wowote leo wala kesho kuwawazia kinyume na kauri yake. Aliyotamka yanabaki kama yalivyo maana Bwana wetu sisi habadililiki badiliki wala hana kigeugeu kama binadamu walivyo[Waebr13:8].

Mungu wetu anaposema haya si kwa Israeli tu bali na kwetu sote tuliompokea Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yetu leo na hata kwa watakaompokea baadaye. Hivyo lazima tumwamini maana yatokayo kwake ni kweli na Amina[1 Wakori.1:19-20; Warumi 9:1-33]

Mungu wetu amejaa kweli na katika hiyo tunapata faraja na imani yetu kuongezeka tukiamini kuwa tunaye Bwana anayetujali katika mahitaji au shida zetu zote. Tunapofahamu hivyo hakuna tena haja ya kutahayari maana tunaye anayetujari kuliko tunavyofikiri. Ni Mungu wetu aliyeahidi na LAZIMA atatimiza.

Yeye hana historia ya kusema uongo wala hatasema uongo- [Waeb.10:23]yeye aliyeahidi ni mwaminifu. Basi na tuipokee ahadi yake ikatusaidie wakati wa mahitaji. Amini mpendwa kuwa Bwana anakuwazia mawazo mema. Katika hitaji lako ambalo umekuwa nalo kwa muda mrefu au mfupi Bwana yupo. Anaweza. Dumu katika imani naye atafanya.

Ubarikiwe sana kwa kufatilia  neo hili.

Tuombeane [Waefe.6:18]


Mzee Shaphat S.K. -  Mwanafunzi wa Yesu 


Comments